Thursday, September 7, 2017

Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana


Mwanasiasa wa upinzani nchni Tanzania Tundu Lissu ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma,katikati mwa Tanzania
Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya Dodoma General.
Hivi karibuni ,mbunge huyo kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA, amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanyauchochezi.
Akithibitisha tukio hilo,kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema " yupo hospitali, bado anajaribu kupambana kuokoa maisha yake"
chanzo na bbc swahili.
Maelezo zaidi kufuata.

No comments:

Post a Comment