Mashindano ya voliboli ya walemavu kuwania ubingwa wa Afrika yameingia katika siku yake ya pili leo mjini Kigali timu ya Morocco ikiwa ya kwanza kujihakikishia tiketi ya robo fainali.Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema timu ya Morocco imeendelea kuonyesha umahiri katika mashindano hayo.
Mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita Morocco imeilima Afrika Kusini seti 3-0.Ushindi huu unafuatia ushindi mwingine wa jana Morocco ilipoizaba Kenya seti 3-0 za 25-21,25-19 na 25-18.
Mchezaji wa Kenya James Mang'erere akakiri kuzidiwa maarifa.Jana usiku pia Rwanda ilikandika Afrika kusini seti 3-0 25-10,25-16 na 25-17.Upande wa wanawake Misri ilichapwa na Kenya seti 3-2 huku Rwanda ikiichalaza DRC seti 3-0.
Mnamo mechi za leo, inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Rwanda na Kenya wanaume, mechi inachezwa usiku huu.
No comments:
Post a Comment