Mwenda pole
hajikwai ,tafsiri ya maneno haya inanipa shauku ya kukimbia mpaka ngambo
kutafuta almasi ya kutatua tatizo langu lakini pia yaweza kuwa dawa ya mtu
yeyote anayependa michezo.
Takribani dakika
tano natembea hadi katikati ya uwanja na kuwaletea mwali mwenye mwendo mkali
atembeapo utadhani ni swala lakini lahasha huyu ni tennesi.
Tennis ni aina ya michezo
inayotekelezwa na watu wawili au wanne wakishindana kwa kupiga mpira mdogo kwa
raketi kwenye uwanja wa tennis. Shabaha ni kupiga mpira kwa upande wa mpinzani
kwa namna inayomshinda kurudisha mpira.
Chanzo chake
kilikuwa wakati wa karne ya 11 huko Ufaransa. Wakati ule wchezaji walipiga kwa
mkono wakuiza “Jeu de Paume” yaa mchezo wa makofi. Baada ya kuenea nchini
Poland watu walianza kutumia raketi badala ya makofi. Michezo hii ilipendwa
sana Uingereza na Ufaransa. Jina "tennis" limetokana na neno la
Kifaransa "tenez!" linalomaanisha "shika!" au
"chukua!".
Katika nusu ya pili ya karne ya 19 imekuwa
michezo ya kupendwa kati ya watu wa tabaka ya juu ya Uingereza
ikasambazwa
katika koloni za Milki ya Uingereza na Marekani. Mashindano makubwa yalianza
huko Wimbledon, Uingereza yanayoendelea hadi leo.
Hadi 1924
tennis ilikuwa michezo kwenye Michezo ya Olimpiki, ikaondolewa na kurudishwa
mwaka 1988. Katika nchi mbalimbali hadi leo ina sifa ya kuwa michezo ya
matajiri lakini katika nchi nyingine inachezwa na watu wa tabaka zote.
Kuna
mashindano makubwa yanayochezwa na timu za kitaifa yanayojulikana kwa jina la
Davis Cup. Uwanja una
umbo la mstatili mwenye urefu wa mita 23.77 (futi 78) na upana wa mita 8.23
(futi 27) kwa wachezaji wawili. Kwa wachezaji wanne upana ni mita 10.97 (futi
36).
Katikati ya
urefu unatenganishwa kwa wavu kuwa na nusu mbili. Mipaka ya uwanja ni mistari
ya nje, wakati mpira unagusa mstari bado uko ndani ya uwanja.
NA RASHIDA IDD.
No comments:
Post a Comment