Tarehe 6 mwezi wa 6 mwaka 2015 katika dimba la Olympia Stadion mjini Berlin BarcelonA
waliwaliza mashabiki wa klabu ya Juventus katika fainali ya Champions League baada ya kuwachapa mabao 3 kwa 1.
Miaka miwili baadae Barcelona walisafiri hadi Italia kuwafuata Ujerumani katika robo fainali ya Champions League na safari hii ilikuwa zamu yao kulia, kipigo cha bao 3 kwa nunge kikawaondoa katika michuano hii.
Miezi 5 baada ya Barca kuondolewa na Juventus hii leo wanakutana tena katika hatua ya makundi ya Champions League na safari hii kula upande una silaha mpya na una silaha kubwa iliyopungua.
Barcelona wanakutana na Juventus huku wakiwa hawana Neymar aliyetimkia PSG lakini uwepo wa Osmane Dembele unawapa matumaini, Juventus Leornado Bonucci amekwenda Ac Millan lakini Douglas Costa ameongezwa kwenye timu.
Msimu uliopita Juventus walipewa nafasi kubwa kubeba kombe la michuano hii kwani kikosi chao kilionekana hatari lakini walikubali kupoteza katika fainali dhidi ya Real Madrid jambo ambalo hawako tayari kulirudia.
Leo Waargentina wawili wanaweza kuamua mchezo, kwani Lioneil Messi ambaye ametoka kufunga hat trick wiki iliyopita anatarajiwa kuibeba Barcelona huku Paulo Dyabala naye akifunga hat trick dhidi ya Genoa.
Ni wazi kwamba wafalme hawa wa Argentina leo wataweka undugu wao pembeni na kila mmoja atakuwa na jukumu la kuibeba klabu yake, Luis Suarez na Gonzalo Higuain pia wanaangaliwa zaidi katika safu ya mbele kuzibeba timu hizi.
Ni mchezo ambao ukiuangalia kwa makini utagundua kwamba wachezaji wengi wanaotegemewa kuleta matokeo wanatokea/ wana asili ya bara la America Kusini.
Cha kufurahisha zaidi kuhusu mpambano huu ni kwamba Barcelona na Juventus wameshakutana mara 13 na katika michezo yote hiyo hakuna mbabe kwani kila mmoja kamfunga mwenzake mara 5 wakasuluhu mara 5 huku kila mmoja akisuluhu mara 3, hivyo leo Nou Camp mbabe kati ya matembo hawa wawili anaweza patikana.
No comments:
Post a Comment