Wednesday, September 20, 2017

Tetemeko laua zaidi ya watu 200 Mexico

Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.
Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea.
''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sekunde thelathini tu, lakini ilionekana kama limedumu daima...'' anasema Daniel Lieberson
Kwa upande wake Natasha Pizzey mwandishi wa habari katika mji huo anasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka..Tunafahamu kuna watu walionusurika katika majengo ya makazi yaliyoporomoka, hatukuwa na uwezo wa kuwaokoa. Kuna mamia ya wafanyakazi wa kujitolea waliokwenda katika eneo la tukio...'' ameongezea kusema
Aidha pia kumetokea madhara mabaya katika majimbo ya jirani ya Morelos na Puebla.
Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90..


Leicester City wawatupa nje Liverpool Kombe la Carabao

Islam Slimani alifunga bao kwa kombora kali na kuwasaidia Leicester kuwalaza Liverpool 2-0 katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la Carabao, ambao pia hufahamika kama Kombe la EFL, uwanjani King Power Jumanne.
Mchezaji huyo wa Algeria alifunga kwa mguu wa kushoto baada ya nguvu mpya Shinji Okazaki kuwaweka Leicester kifua mbele.
Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kuondolewa uwanjani.
Okazaki aliingia uwanjani na kuwaongezea nguvu Leicester na kufunga kutoka kwa pasi safi iliyotoka kwa Vicente Iborra.
Alex Oxlade-Chamberlain na Dominic Solanke walionunuliwa na Liverpool majuzi wote walipoteza nafasi nzuri za kufunga.
Kwingineko Roy Hodgson alipata ushindi wake wa kwanza Crystal Palace wakiwa nyumbani dhidi ya Huddersfield.
Bristol City nao waliwashangaza Stoke City.
Tottenham nao walichukua dakika 65 kuwapangua Barnsley uwanjani Wembley nao Leeds wakawalaza Burnley kwa mikwaju ya penalti uwanjani Turf Moor.
Liverpool watasafiri tena Leicester kwa mechi ya Ligi ya Premia siku ya Jumamosi, mechi ambayo itaanza saa moja unusu jioni saa za Afrika Mashariki.chanzo bbc swahili

Haye ataka kukipiga kwa mara nyingine na Bellew

Bondia David Haye amesema yupo tiyari kurudia mpambano na Tony Bellew.
Mpambano wao wa raundi 11 uliishia raundi ya 6 walipokutana mwezi Machi.
Haye alipigwa ndani ya raundi ya sita kwa makonde ya mfululizo yaliyompeleka chini.
Ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba'' imechukua miezi kadhaa ya majadiliano na sasa ni muda wa kwenda tena ulingoni.

Hakuna tarehe wala sehemu kamili mpambano huo utakapofanyika, lakini baadhi ya taarifa zinasema utafanyika Disemba 17, kwenye uwanja wa London O2.
Haye alifanyiwa upasuaji baada ya kuchapwa vibaya na Bellew mzaliwa wa Liverpool na tokea kupona kwake amekuwa akifanya mazoezi na walimu wake Shane McGuigan

Monday, September 18, 2017

Serikali ya Tanzania yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra

Shughuli zimeanza tena katika mgodi mkubwa zaidi wa madini ya almasi nchini Tanzania, licha ya mzozo na serikali ya Tanzania, ambayo ilikamata bahasha iliyokuwa na almasi kwenye uwanja wa ndege.

Shughuli katika mgodi wa Williamson zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa siku nne.
Wiki moja iliyopita hisa kwenye kampuni ya Uingereza ya Petra zilishuka kwa asilimia 7, baada ya almasi zake kuzuiwa kusafirishwa kutoka nchi Tanzania, ambapo pia wafanyakazi wake kadha walihojiwa na mamlaka za nchi hiyo.
Mamlaka zilikamata bahasha iliyokuwa na almasi ambayo hadi sasa haijaachiliwa.
Mazungumzo ya kampuni na serikali kuhusu suala hilo yanaendelea, kwa kujibu wa kampuni ya Petra.
Kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuchimba almasi nchi Tanzania inalaumiwa kwa kuzusha thamani ya almasi zake.
Serikali inasema kuwa Petro iliandika mzigo huo kuwa wa thamani ya dola milioni 14.6 wakati thahamia yake halisi ilikuwa dola milioni 29.5.
Petro ilikana madai hayo, ikisema kuwa serikali ndiyo inahusika kwa kuthibitisha thamani kama hiyo.
Mgodi wa Williamson ulio kaskazini magharibi mwa Tanzania unamilikiwa na Perto kwa asilimia 25 huku serikali ya Tanzania ikimiliki asilimia 25.chanzo na bbc swahili

Fury aomba hukumu ya kufungiwa ndondi kuondolewa

Bondia wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury ameomba kuondolewa adhabu ya kutoshiriki mchezo huo ikiwa ni karibia mwaka mzima tokea kufungiwa.
Fury mwenye miaka 29, hajapigana tokea alipomtwanga Wladimir Klitschko Novemba 2015.
Mahakama ilisogeza mbele kusikilizwa kwa kesi yake na mpaka sasa bado haijapangwa tena.
''Ni kwa muda gani nitakaa nje ya ulingo?'' Fury aliandika kwenye mtandao wa Twitter.
''Safisheni jina langu na mniache nirejee kufanya kile ninachokipenda.Sina kosa, niachieni huru!''
Fury atapaswa kuhojiwa na bodi ya kuzuia matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni na baada ya hapo watatoa uamuzi.chanzo na bbc swahili

Rooney ahukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili

Nahodha wa zamani watimu ya taifa ya England Wayne Rooney amehukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili sambamba na kufanya kazi za jamii kwa saa 100.



Rooney 31, alikamatwa kwenye kitongoji cha Wilmslow, Cheshire kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa Rooney pia atalipa faini ya Pauni 170 kwa kosa hilo.
''Nimekubali kosa langu na nimeomba radhi kwa familia, klabu yangu ya Everton, mwalimu na sasa ni zamu ya mashabiki.Ninaomba radhi kwa kitendo kile.'' alisema Rooney baba wa watoto watatu. 1.
Mchezaji huyo aliyezaliwa katika jiji la Liverpool alijiunga na Everton klabu yake ya utotoni akitokea Manchester United miaka 13 baada ya kuondoka.chanzo bbc swahili

KOCHA NJOMBE MJI ANG’ATUKA BAADA YA KUPIGWA MECHI TATU MFULULIZO

TIMU ya Njombe Mji imepata pigo baada ya kocha wake Mkuu, Hassan Banyai kung’atuka kufuatia matokeo mabaya katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
Njombe Mji FC imefungwa mechi zote tatu za mwanzo za Ligi Kuu, mbili nyumbani Uwanja wa Saba Saba dhidi ya Tanzania Prisons 2-0 na Yanga SC 1-0 kabla ya kuchapwa 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Na kabla ya kuingia kwenye mchezo wa nne dhidi ya Ruvu Shooting Septemba 23, mwaka huu, leo Njombe Mji imetoa taarifa ya kutengana na kocha wake aliyeipandisha timu Ligi Kuu msimu huu.
Afisa Habari wa Njombe Mji FC, Solanus Mhagama amesema kwamba kwa kipindi hiki, aliyekuwa Kocha Msaidizi, Mrage Kabange ndiye ataiongoza timu hadi hapo uongozi utakapotoa tamko longine.
Njombe Mji imemshukuru Banyai kwa mchango wake kwenye timu ikiwemo kuipandisha Ligi Kuu na kumtakia kila la heri huko aendako.
Mhagama amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani mwishoi mwa wiki.

KADO AREJEA KAZINI MTBWA BAADA YA KUPONA GOT

BENCHI la Ufundi la Mtibwa Sugar ya Morogoro limepokea habari njema kufuatia kupona kwa kipa wake namba moja, Shaaban Hassan Kado aliyeumia mwezi uliopita.
Kado aliumia goti baada ya kugongana na mshambuliaji wa Simba, John Bocco katika mchezo wa kirafiki Agosti 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na tangu hapo amekuwa nje kwa matibabu.

Lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Kado aliyerejea Mtibwa Sugar msimu huu kutoka Mwadui FC ya Shinyanga, amesema kwamba amepona kikamilifu na yupo tayari kurejea Kado amesema kwamba madaktari waliokuwa wanamtibu wamemruhusu kujumuika na wachezaji wenzake kuanza mazoezi baada ya kuridhishwa na maendeleo yake.

“Kwa kweli nimepona kabisa na niko fiti kwa ajili ya kuitumikia timu yangu, mwanzoni nilipewa ruhusa ya kufanya mazoezi mepesi, ila kwa sasa nimeanza mazoezi kikamilifu, na ninaweza kusema niko fiti kwa ajili ya mapambano,’amesema Kado.


Kurejea kwa Kado ni habari njema kwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao wana makipa wengine watatu wa kikosi cha kwanza, Abdallah Makangana ‘Dida’, Benedictor Tinocco na Abutwalib Msheri.
Na baada ya kupona na kurejea uwanjani kwa Kado uwanjani,
 Mtibwa Sugar inabaki na wachezaji wawili majeruhi kikosini, ambao ni beki Hassan Isihaka ambaye tayari ameanza mazoezi mepesi na kiungo Haruna Chanongo anayesumbuliwa na maumivu ya goti pia.
.  

Thursday, September 14, 2017

Morocco na Kenya zawika voliboli ya walemavu Rwanda

Mashindano ya voliboli ya walemavu kuwania ubingwa wa Afrika yameingia katika siku yake ya pili leo mjini Kigali timu ya Morocco ikiwa ya kwanza kujihakikishia tiketi ya robo fainali.Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema timu ya Morocco imeendelea kuonyesha umahiri katika mashindano hayo.
Mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita Morocco imeilima Afrika Kusini seti 3-0.Ushindi huu unafuatia ushindi mwingine wa jana Morocco ilipoizaba Kenya seti 3-0 za 25-21,25-19 na 25-18.
Mchezaji wa Kenya James Mang'erere akakiri kuzidiwa maarifa.Jana usiku pia Rwanda ilikandika Afrika kusini seti 3-0 25-10,25-16 na 25-17.Upande wa wanawake Misri ilichapwa na Kenya seti 3-2 huku Rwanda ikiichalaza DRC seti 3-0.
Mnamo mechi za leo, inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Rwanda na Kenya wanaume, mechi inachezwa usiku huu.

Kenya na Tanzania zashuka orodha ya Fifa

Timu za soka za mataifa ya Kenya na Tanzania zimeshuka kwenye orodha ya kila mwezi ya viwango vya soka duniani inayotolewa na Fifa.
Harambee Stars imeshuka nafasi sita hadi nambari 88 duniani, Taifa Stars nao wakashuka nafasi tano hadi nambari 125.
Rwanda wamepanda nafasi moja hadi nambari 118, lakini DR Congo wameshuka nafasi 14 hadi nambari 42.

Uganda wamepanda nafasi mbili na wanashikilia nafasi ya 71.
Burundi wamepanda nafasi tatu hadi nambari 129.
Misri wanaongoza Afrika wakiwa katika nafasi ya 30 baada ya kushuka nafasi 5.
Somalia na Eritrea wanashika mkia wakiwa nafasi ya 206 kwa pamoja, wakiwa hawana alama zozote.
Ushelisheli wanawafuata kutoka nyuma wakiwa nafasi ya 190 baada ya kupanda nafasi 4.
Nafasi dunianiTaifaImeshuka au Kuipanda
30Misri-5
31Tunisia3
33Senegal-2
42Congo DR-14
44Nigeria-6
45Cameroon-10
49Burkina Faso
52Ghana-2
54Côte d'Ivoire0
56Morocco4
62Algeria-14
Ujerumani sasa ndio taifa bora zaidi kwa soka duniani baada ya kuwapita Brazil ambao sasa wanashikilia nafasi ya pili.
Nafasi dunianiTaifaImeshuka/Kupanda
1Germany1
2Brazil-1
3Portugal3
4Argentina-1
5Belgium4
6Poland-1
7Switzerland-3
8France2
9Chile-2
10Colombia-2

Paul Pogba: Nyota wa Man United kukaa nje wiki sita kutokana na jeraha

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje ya uwanja kwa kati ya mwezi mmoja na wiki sita baada yake kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne.

Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano.
Inafahamika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja.
Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool ugenini 14 Oktoba.
Meneja wa United Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari Ijumaa.
Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.
Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.
Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.
Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka ujao.CHANZO BBC SWAHILI.

Wednesday, September 13, 2017

Jembe la Azam linavyoipalilia Yanga

Wakati wa dirisha kubwa la usajili lilipokuwa linaendelea mwezi uliopita, nilikuwa najiuliza kwa nini Yanga wang’ang’anie kuwa Gadiel Michael ni mchezaji wao, huku yeye mwenyewe akiikataa Azam ghafla na kutaka kuondoka, Azam nao wakisema kuwa bado ni mchezaji wao halali kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mchezaji huyu hivi sasa amegeuka kuwa lulu, kati ya mabeki wanaocheza nafasi za pembeni kutokana na aina ya uchezaji wake

Gadiel aliona tayari kuna ufinyu wa namba katika kikosi cha Azam kutokana na kuwa na Mzimbabwe Bruce Kangwa hivyo ilipokuja ofa ya Yanga aliona bora aondoke.
Azam ilikubali kumuachia kwa kuweka dau dogo ambalo Yanga walitoa kama fidia na mchezaji huyo akajiunga na klabu hiyo ya Jangwani.
Kama bado angekuwa yupo mikononi mwa kocha wa Azam Cioba, inawezekana leo asingekuwa huyu tunayemuona, itakuwa aliona mbali zaidi na ndio maana akataka kuondoka, kikubwa ni kumuomba Mungu afanikiwe zaidi.
Ufalme wa Oscar Joshua ulichukuliwa na Mwinyi Haji, ufalme wa Mwinyi Haji umechukuliwa na Gadiel Michael hilo halina ubishi.
Michael amekuwa mchezaji wa adhimu tayari katika kikosi hicho kutokana na umahiri wake wa kumudu kuicheza namba hiyo.
Haji ana kazi kubwa ya kumshawishi Lwandamina ampe nafasi la sivyo yatamkuta kama yaliyomkuta Joshua kipindi yeye anacheza. 
Mechi ya Stars dhidi ya Lesotho ndiyo ilikuwa mechi iliyofanya beki huyu apate namba ya kudumu Stars.
Alionyesha kiwango cha juu katika kukaba na kupeleka mashambulizi huku kikiwa ndio kitu sahihi katika mpira wa sasa (Modern football).
Mayanga ameonyesha kumuamini kijana huyu kutoka na kumpa nafasi kila anapomuita, Michael naye hajawahi kumuangusha.
Amezidi kukomaa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, amekuwa ni mchezaji mbishi dhidi ya washambuliaji pindi wanapokuja kushambulia lango lao.
Anapambana sana katika kuzuia mashambulizi lakini pia ni mchezaji ambaye anaweza kupeleka mashambulizi kwa spidi na kupiga krosi ambazo zinaweza kuzaa mabao.
Pia ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo hasa za pembeni, hii ni kutokana na jinsi ambavyo anaweza kupiga krosi, hivyo faulo za pembeni anazitumia kama krosi zake.
Kwa umri alionao hivi sasa na kiwango ambacho anakionyesha, dhahiri kwamba anajipa wakati mwepesi katika kuingia kwenye kugombea tuzo ya mchezaji bora Chipukizi.
Kupata kwake namba katika kikosi cha Yanga na Stars, hii ni chachu kubwa kwani hata kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ baada ya kufanya vizuri akiwa na Simba pamoja na Stars alijikuta akipata tuzo hiyo.



Shabiki aingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke Mbappe wa PSG

Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.

Kisa hicho kilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo siku ya Jumanne muda mfupi baada ya wageni hao kuwafunga Celtic bao la tano.
PSG pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo.
Kesi hiyo itaangaziwa na kitengo cha maadili na nidhamu katika shirikisho la Uefa tarehe19 Octoba
Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.
Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri.
Inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya.chanzo bbc swahili
Mwenda pole hajikwai ,tafsiri ya maneno haya inanipa shauku ya kukimbia mpaka ngambo kutafuta almasi ya kutatua tatizo langu lakini pia yaweza kuwa dawa ya mtu yeyote  anayependa  michezo.







Takribani dakika tano natembea hadi katikati ya uwanja na kuwaletea mwali mwenye mwendo mkali atembeapo utadhani ni swala lakini lahasha huyu ni tennesi.
 Tennis ni aina ya michezo inayotekelezwa na watu wawili au wanne wakishindana kwa kupiga mpira mdogo kwa raketi kwenye uwanja wa tennis. Shabaha ni kupiga mpira kwa upande wa mpinzani kwa namna inayomshinda kurudisha mpira.
Chanzo chake kilikuwa wakati wa karne ya 11 huko Ufaransa. Wakati ule wchezaji walipiga kwa mkono wakuiza “Jeu de Paume” yaa mchezo wa makofi. Baada ya kuenea nchini Poland watu walianza kutumia raketi badala ya makofi. Michezo hii ilipendwa sana Uingereza na Ufaransa. Jina "tennis" limetokana na neno la Kifaransa "tenez!" linalomaanisha "shika!" au "chukua!".

Katika nusu ya pili ya karne ya 19 imekuwa michezo ya kupendwa kati ya watu wa tabaka ya juu ya Uingereza 
ikasambazwa katika koloni za Milki ya Uingereza na Marekani. Mashindano makubwa yalianza huko Wimbledon, Uingereza yanayoendelea hadi leo.


Hadi 1924 tennis ilikuwa michezo kwenye Michezo ya Olimpiki, ikaondolewa na kurudishwa mwaka 1988. Katika nchi mbalimbali hadi leo ina sifa ya kuwa michezo ya matajiri lakini katika nchi nyingine inachezwa na watu wa tabaka zote.

Kuna mashindano makubwa yanayochezwa na timu za kitaifa yanayojulikana kwa jina la Davis Cup.Uwanja una umbo la mstatili mwenye urefu wa mita 23.77 (futi 78) na upana wa mita 8.23 (futi 27) kwa wachezaji wawili. Kwa wachezaji wanne upana ni mita 10.97 (futi 36).

Katikati ya urefu unatenganishwa kwa wavu kuwa na nusu mbili. Mipaka ya uwanja ni mistari ya nje, wakati mpira unagusa mstari bado uko ndani ya uwanja.
 NA RASHIDA IDD.

Huu ndio mkwanja wanaovuta Singida United kutoka kwa wadhamini wote

Timu ya Singida United imerejea kwenye ligi msimu huu baada ya kusota bondeni kwa muda mrefu, lakini wamerejea kwa kishindo kwa kuwa ni miongoni mwa vilabu ambavyo mfuko wao wa salio umetuna kutokana na pesa za wadhamini.
Singida wana wadhamini rasmi watatu (YARA, SportPesa na Puma) wana wadau pia wanaowawezesha kama NMB Bank, DTB Bank na Oryx wote hao wanaingiza mtonyo ndabi ya Singinda United huku klabu hiyo ikitarajia kutangaza wadhamini wengine wawili hivi karibuni.
Mkurugezi wa Singida United Festo Sanga ametaja wadhamini na wadau wote wa klabu yao na kiasi cha pesa wanachowapa kwa mwaka.
“Tuna udhamini mkubwa kutoka YARA ambao wanatoa zaidi ya shilingi milioni 300 za Tanzania kwa mwaka mmoja, tuliwafuata na walikuwa mwisho kwenye budget yao kwa hiyo wametuahidi kwenye budget ijayo mambo yatakuwa mazuri zaidi,” Festo Sanga.
Mmdhamini wetu mwingine ni SportPesa ambaye anatoa zaidi ya shilingi milioni 250 kwa mwaka. Udhamini mwingine tumepata kutoka Puma wa zaidi ya shilingi milioni 120.”
“Oryx ni wadau wetu (sio wadhamini) wametupa zaidi ya shingi milioni 100,  hawataki kujionesha kama wanatudhamini kwa sababu program yao kubwa ya kuidhamini Singida United itaanza mwaka ujao. DTB Bank ni wadu wetu wengine waliotupa zaidi ya shilingi milioni 20, NMB wametupa milioni 10 kwa ajili ya kui-support klabu.”
Ukifanya hesabu ndogo hapo utagundua Singida United wanatengeneza zaidi ya shingi milioni 800 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini na wadau wao sawa na kiasi inachopata klabu ya Simba kutoka kwa wadhamini wao SportPesa kwa mwaka wa kwanza wa udhamini huo
NMB na DTB ni kambuni mbili zenye ushindani wa kibiashara lakini wote wanaiunga mkono Singida United, hawa sio wadhamini ni wadau tu hawana mkataba wa udhamini na klabu hiyo.