Shirikisho la soka barani Afrika CAF
limetoa orodha ya wachezaji watano watakaoshindania tuzo ya mchezaji
bora wa mwaka 2016, kwa wachezaji wa jumla na wachezaji wa ligi za
barani Afrika.
Wanaoshindania tuzo ya jumla ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka ni:- Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borrusia Dortmund
- Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester
- Sadio Mane wa Senegal na Liverpool
- Mohamed Salah wa Egypt na Roma
-
Islam Slimani wa Algeria na Leiceste.Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea soka ya kulipwa
Ubelgiji Mbwana Ally Samatta ni miongoni mwa wachezaji 30 waliokuwa
wameteuliwa kushindania Tuzo ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF)
ya Mchezaji Bora wa Afrika katika awamu ya kwanza kabla ya wachezaji hao
kupunguzwa hadi watano.
Mkenya Victor Wanyama ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Tottenham alikuwa pia ameteuliwa, pamoja na Yannick Bolasie wa DR Congo anayechezea Everton
.
Wachezaji watakaoshindania orodha ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka
anayecheza ligi za Afrika ni:
- Khama Billiat wa Mamelodi Sundowns na Zimbabwe
- Keegan Dolly wa Mamelodi Sundowns na South Africa
- Rainford Kalaba wa TP Mazembe na Zambia
- Hlompho Kekana wa Mamelodi Sundowns na South Africa
- Denis Onyango wa Mamelodi Sundowns na Uganda
-
Wachezaji hao waliamuliwa kwa kura zilizopigwa na Kamati ya
Wanahabari ya CAF, Kamati ya Kiufundi na Ustawishaji ya CAF na nusu ya
wanachama wa jopo la wataalamu 20.
- Samatta afurahia kushindania tuzo ya Afrika
- Samatta na Wanyama kushindania tuzo ya CAF
- Samatta asaidia klabu yake kufunga
No comments:
Post a Comment