Huku maeneo mengi ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa
kupita kiasi, Uholanzi ina tatizo tofauti . Uchache wa wafungwa .
Katika kipindi cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake
na mengine zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili
liliwezekana - na kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya
mahabusu na katika jengo zima . Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao
cha jioni . Mwnamume mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliofungwa juu.
"Hawawezi
kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel,
naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko
kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "Lakini wanaweza kuazima visu vidogo
vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini"
Baadhi
ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba
watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni
moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya
kawaida mara baada ya kufunguliwa.Katikka magereza ya Uholanzi tuanaangalia kila mmoja ," anasema Van der Spoel.
"
Kama mtu fulani ana matatizo ya mihadarati tunatibu hali yake, kama ni
wenye hasira tunawapatia ushauri wa kudhibiti hasira zao , kama wana
matatizo ya pesa tunawapatia ushauri nasaha. Kwa hiyo tunajaribu
kuondoa kile kinachosababisha mtu afanye uhalifu . Mfungwa mwenyewe
lazima awe na utashi wa kubadilika lakini njia yetu imewafaa sana. Kwa
zaidi ya miaka 10 , kazi yetu imeboreka zaidi na zaidi.''
Wafungwa
wanaofuata maelekezo hatimaye hupewa kifungo cha miaka miwili na
msururu wa mafunzo katika mpango wa kuwarejesha katika hali ya kawaidi .
Chini ya 10% hurejea gerezani baada ya kuachiliwa huru.
Hewa
safi ni muhimu kwa hiyo wafungwa huruhusiwa kutembea wakisindikizwa hadi
maktaba , kwenye kliniki ama mgahawa na hilo huwasaidia kuendelea na
maisha ya kawaida punde wanapomaliza kifungo cha gerezani.chanzo na bbc swahili

No comments:
Post a Comment