Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amepiga chini uvumi wa ujio wa
kiungo mkabaji Meshack Chaila kutoka Zesco United baada ya kusambaa kwa
habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba kocha huyo amependekeza Yanga
kumsajili mchezi huyo
.
Lwandamina ameniambia hakuna mchezaji ambaye atakuja kutoka Zesco
lakini akakiri kuwa kama uongozi wa Yanga watakubaliana na nyota huyo
yeye hana tatizo.
“Hakuna mchezaji anayekuja kutoka Zambia, nimesikia hizo tetesi
hakuna yeyote aliyeniambia kuhusu Chaila. Kama watazungumza nae
atatakiwa kufanya uamuzi wake kwa maisha yake ya badae,” Lwandamina
akaziua tetesi za Chaila kutua Bongo kama ambavyo imekuwa isemwa siku za
hivi karibuni.
Hata ukimpa nafasi moja ya kuchagua mchezaji mmoja kutka Zesco United
jamaa amesema hakuna hata mchezaji mmoja atakaemleta kutoka kwenye
klabu yake ya zamani.
“Wote ni wachezaji wazuri lakini inategemea na mahitaji ya timu hii,
mapungufu yaliyopo kwenye klabu ndiyo yanaamua ni mchezaji wa aina gani
anahitajika kwa wakati huo
.
Tofauti ya ligi ya Tanzania na Zambia
Lwandamina amesema anafahamu kidogo kuhusu soka la Tanzania lakini
kiushindani huwezi kulinganisha na Zambia kwasababu wao tayari wako
mbele zaidi ya Tanzania
.
“Ligi ya Tanzania inaushindani wake lakini huwezi kulinganisha na
Zambia kwasababu wao wapo level nyingine kwahiyo hapa tunatakiwa
kuangalia kwa nini ligi ipo hapo ilipo halafu twende mbele zaidi.”
Malengo yange ndani ya Yanga
Anataka kuipa Yanga mafanikio zaidi ya yale ambayo wanayo sasa, anasema hiyo ndiyo changamoto iliyopo mbele yake.
“Nataka kupata mafanikio zaidi waliyonayo sasa, kitu muhimu kwenye
maisha ni kujua wapi utaanzia na wapi unataka kufika na utafikaje.
No comments:
Post a Comment