Sunday, November 27, 2016

wakurugenzi 5 ATCL kubwagwa


BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imeeleza kuongezeka kwa makusanyo ya shirika hilo katika kipindi kifupi cha uendeshaji wake kutokana na kudhibitiwa kwa mapato na matumizi
.
Aidha bodi hiyo imeagiza kuwaondoa wakurugenzi watano na baadhi ya mameneja katika nafasi zao kwa kuwa wengi wao wana viwango vya chini vya elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao hivyo kusababisha utendaji wa kazi kuwa dhaifu.

Kutokana na hatua hiyo, bodi hiyo imemuagiza Ofisa Mtendaji Mkuu kutangaza nafasi zote za wakurugenzi na mameneja zilizo wazi na zile zenye wafanyakazi wenye utendaji dhaifu kwa kuzingatia muundo wa muda uliopitishwa na bodi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo ya ATCL, Emmanuel Korosso alipokuwa anazungumzia masuala yanayoihusu kampuni hiyo.

Akizungumzia kuimarika kwa makusanyo, Korosso alisema; Katika kipindi kifupi tangu kuanza kwa safari za ndege mpya tumeweza kudhibiti mapato na matumizi na kumekuwa na ongezeko la mapato ya uzito wa ziada wa mizigo.

Kuhusu kuondolewa kwa wakurugenzi na mameneja, Mwenyekiti huyo wa bodi alisema bodi hiyo imeagiza kuwa wakurugenzi na mameneja waliokuwa wamethibitishwa kazini lakini hawana sifa kuondolewa katika nafasi zao na kupangiwa majukumu mengine kulingana na sifa zao.

Mwenyekiti huyo wa bodi alisema muundo wa muda unataka uwepo wa wakurugenzi watatu tu katika uendeshaji wa kampuni hiyo.

Akizungumzia baadhi ya maboresho, Korroso alisema katika matumizi ya tiketi za bure au zilizopunguzwa bei, bodi imeagiza Menejimenti ya ATCL kusimamisha kwa muda Mkataba wa Hiari baina ya Menejimenti na wafanyakazi na sasa watapewa tiketi za bure na tiketi yenye punguzo mara moja kwa mwaka kama stahili ya likizo.

Kuhusu idadi ya wafanyakazi Korosso alisema hivi sasa shirika hilo linao wafanyakazi 221 na wanalenga wakiwa na ndege zao zote watakuwa na wafanyakazi 350.

Alisema baada ya kupokea ndege mpya mbili aina ya Bombardier Q400 na kuanza safari Oktoba 14 mwaka huu katika kumekuwepo na changamoto ya ucheleweshaji wa ndege na pia kutokutoa huduma kwa maeneo yaliyopaswa kufikiwa.chanzo na habari leo

Rais Magufuli atunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya wa JWTZ Ikulu Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kundi la 59/15 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.



Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya  Ikulu.



Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.
 
Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la gwaride la kimyakimya.



Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.



Aidha, Rais Magufuli alisema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo Viongozi wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.
 
"Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu" alisema Rais Magufuli.
.



Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.chanzo na mpekuzi
 

Lowassa Awajibu wanasiasa waliodai ni mgonjwa na atakufa

Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.
 

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.
 

Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.

Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.
 

“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” alisema.
 

Pamoja na hayo, Lowassa aliwataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.
 

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
 

Baadhi ya wanasiasa, hususani wale waliokuwa wakimpinga, walijaribu kuionyesha na hata kuiaminisha jamii kwamba mwanasiasa huyo ni mgonjwa na hafai kuongoza nchi.
 

Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.

Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.
 

Miongoni mwa wapinzani wake ni baadhi ya wanasiasa wakubwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo viongozi waliosikika katika majukwaa ya kampeni  mwaka jana wakiwashawishi wananchi kutomchagua Lowassa kwakuwa hata akipata urais hatotawala muda mrefu atakufa.
 

Wapo waliokwenda mbali na kusikika wakimwambia Lowassa Ikulu si wodi ya wagonjwa, hivyo hafai kupatiwa nafasi ya urais kulingana na afya aliyonayo.
 

Mikutano ambayo Lowassa ameitumia kuzungumzia suala hilo, inafanyika nchi nzima pamoja na kuwahusisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama.
 

Uwepo wa Lowassa katika mikutano hiyo imesababisha watu wengi kukusanyika wakitaka kumuona.chanzo na mpekuzi

Lwandamina amtosa Misheck Chaila

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amepiga chini uvumi wa ujio wa kiungo mkabaji Meshack Chaila kutoka Zesco United baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba kocha huyo amependekeza Yanga kumsajili mchezi huyo
.
Lwandamina ameniambia hakuna mchezaji ambaye atakuja kutoka Zesco lakini akakiri kuwa kama uongozi wa Yanga watakubaliana na nyota huyo yeye hana tatizo.

“Hakuna mchezaji anayekuja kutoka Zambia, nimesikia hizo tetesi hakuna yeyote aliyeniambia kuhusu Chaila. Kama watazungumza nae atatakiwa kufanya uamuzi wake kwa maisha yake ya badae,” Lwandamina akaziua tetesi za Chaila kutua Bongo kama ambavyo imekuwa isemwa siku za hivi karibuni.

Hata ukimpa nafasi moja ya kuchagua mchezaji mmoja kutka Zesco United jamaa amesema hakuna hata mchezaji mmoja atakaemleta kutoka kwenye klabu yake ya zamani.
“Wote ni wachezaji wazuri lakini inategemea na mahitaji ya timu hii, mapungufu yaliyopo kwenye klabu ndiyo yanaamua ni mchezaji wa aina gani anahitajika kwa wakati huo
.

Tofauti ya ligi ya Tanzania na Zambia
Lwandamina amesema anafahamu kidogo kuhusu soka la Tanzania lakini kiushindani huwezi kulinganisha na Zambia kwasababu wao tayari wako mbele zaidi ya Tanzania

.
“Ligi ya Tanzania inaushindani wake lakini huwezi kulinganisha na Zambia kwasababu wao wapo level nyingine kwahiyo hapa tunatakiwa kuangalia kwa nini ligi ipo hapo ilipo halafu twende mbele zaidi.”


Malengo yange ndani ya Yanga
Anataka kuipa Yanga mafanikio zaidi ya yale ambayo wanayo sasa, anasema hiyo ndiyo changamoto iliyopo mbele yake.

“Nataka kupata mafanikio zaidi waliyonayo sasa, kitu muhimu kwenye maisha ni kujua wapi utaanzia na wapi unataka kufika na utafikaje.

Shinji Kagawa anaelezea future yake ndani ya Borussia Dortmund


Mchezaji huyu mwenyr miaka 27 anahushishwa sana na kurudi kwenye ligi ya nchini kwao Japan hasa kujiunga na club ya Yokohama F Marinos
. Mchezaji huyu wa zamani wa Man United na Cerezo Osaka amekubali kwamba ana wakati mgumu ndani ya Ujerumani kwa miezi michache iliyopita lakini bado anaimani na mazoezi anayofanya yatamrudisha kwenye kikosi cha kwanza
.
Alivyoulizwa kuhusu kuachana na club hiyo ili apate nafasi ya kucheza Kagawa alijibu,“Nataka kuonyesha kwamba naweza kucheza mechi hapa nitaonyesha kila kitu nilichokua nacho.

 Nilihitaji kufunga haya magoli na kutoa assist ili niendelee kujiamini. Hii mechi imekua muhimu sana kwangu. Najua nahitaki kufanya mazoezi sana ili niendelee kuwa bora zaidi”

Salamu za Rambirambi za Rais Magufuli Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016. Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu
.

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.
 
Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.
 
 
Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."
 

Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina
 

Serikali yampokonya Sumaye shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33


Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.
 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.
 

“Oktoba 28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati namba 53086.Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” amesema Hapi.
 


Sumaye ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anamiliki mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es Salaam.
 

Baada ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo, Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo.

Sumaye ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anamiliki mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es Salaam.
 

Kwa sababu hati yake imeshabatilishwa na akibainika kufanya chochote vyombo vya dola vitachukua nafasi yake.
 

“Vyombo vya ulinzi na usalama watakuwapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili halitafanyiwa shughuli zozote, isipokuwa baada ya taratibu za manispaa zitakapofanyika,” amesisitiza Hapi.

Amesema amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa na mgogoro wa shamba hilo wafikiriwe.

Februari 5 mwaka huu, akiwa Morogoro, Rais John Magufuli aliwataka watu wote waliotelekeza mashamba kuyaendeleza, la sivyo atawanyang’anya na kuwapa wananchi

Saturday, November 26, 2016

Afrika yamuomboleza Fidel Castro

Habari za kifo cha Fidel Castro zimeibua hisia za majonzi na huzuni katika maeneo mengi Afrika, hasa kutokana na alivyolifaa bara hili.

Alikuwa mtu aliyekuwa mfano wa kuigwa katika harakati za baada ya uhuru kote barani kwamba wakati mmoja alijielezea kama "sababu nzuri zaidi ya kuwepo kwa binadamu".

Uhusiano wake wa karibu hususan na taifa la Afrika kusini - na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi - umekuwa ukiheshimiwa kwa kiasi kikubwa.

Wanajeshi wengi wa Cuba walipoteza maisha yao mbali na nchi yao katika nchi kama vile Angola, wakipigana vita vya ukombozi wa Afrika.

Alisaidia pia wapiganiaji uhuru Msumbiji, kando na kufadhili ujenzi wa miradi mingi ya kuwafaa wananchi mataifa mbalimbali barani Afrika.

Baadhi wanaamini kwamba wakati watu muhimu wa karne ya 20 wanapokumbukwa, ni mmoja wa wanaofaa kukumbukwa.

Wakati wa kutolewa kwa usaidizi wa kimataifa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola katika mataifa ya magharibi mwa Afrika, Fidel Castro, aliwatuma takriban madaktari 300 wa ziada na wauguzi katika mataifa yaliyoathiriwa
.
Pia alisema kuwa Cuba iko tayari kusaidiana na Marekani katika masuala ya maslahi ya amani ya dunia.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya rais Obama kuwataka Wamarekani kuepuka kupotosha ukweli juu ya Ebola.

Katika kipindi cha miongo kadhaa, Castro alituma madaktari wa Cuba katika nchi za kigeni kuwatibu maskini wakiwemo wakazi wa bara la Afrika
.
Mbali na Matibabu mapenzi ya Castro kwa Afrika yalidhihirika kusini mwa Afrika pale ilipoingilia katika katika vita vya Angola suala lililobadili sababu ya historia.

Binafsi Castro aliongoza harakati za kivita katika Cuito Cuanavale manamo mwaka 1988 ambapo majeshi ya Cuba yalishinda jeshi la Afrika Kusini na matokeo yake majeshi ya Afrika Kusini hayakuondoka Angola pekee bali Namibia pia ilifanikiwa kupata uhuru wake.

Nelson Mandela binafsi alisema kuachiliwa kwake kutoka gerezani na kushindwa kwa ubaguzi wa rangi kulitokana na matukio ya Cuito Cuanavale
.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni miongoni mwa viongozi wa kwanza wa nchi mbalimbali duniani waliotuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Fidel Castro.

"Rais Castro alijihusisha na vita vyetu dhidi ya utawala wa ubaguziw a rangi. Aliwahimiza raia wa Cuba kuungana nasi katika vita vyetu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi," amesema.

Afrika Kusini ilipojipatia uhuru 1994, Cuba na Afrika Kusini chini ya Rais Castro na Rais Mandela zilikuwa na urafiki wa karibu na wa dhati.


Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Dlamini Zuma pia ametuma rambirambi, kupitia Twitter ambapo amesema Umoja wa Afrika "unasimama kwa pamoja, kama ilivyo kawaida, na watu wa Cuba wanapoomboleza kufuatia kifo cha kiongozi wao Fidel Castro".chanzo na bbc swahili

Wednesday, November 23, 2016

Dar Mpya ya Makonda: Takukuru kumsaidia Makonda kuondoa migogoro ya ardhi Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku 10 jijini Dar es salaam ambapo Jumatano hii akiwa wilayani Ilala amesema hataweka saini katika nyaraka za ardhi hadi zipitie na Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru].
Akiongea na watumishi wa Halmashauri wa Manispaa Ilala, RC Makonda amesema watumishi wengi wa ardhi wasiowaaminifu wamekuwa wakisababisha migogo mingi ya ardhi
.
“Kuanzia sasa sitaweka sahihi katika nyaraka zozote za ardhi zitakazofika ofisini kwangu hadi zipitie Takukuru zichunguzwe nimegundua kumekuwa na usanii katika uuzwaji wa viwanja,”alisema.

Makonda aliongeza kuwa anazo nyaraka za watendaji waliokuwa wakifanya uchakachauji huku akiwataka watendaji hao kufanya kazi na watu waridhike.

Alisema wataalamu wa kupima ardhi huacha maeneo na kudai kuwa ni meneo yenye bonde au mto huku baadae wakiyauza au hata kudai vimeisha na baadaye kuyatumia kwa manufaa yao na wakati mwingine maofisa hao kubadilisha mafaili ili wauze kwa watu tofauti.

Kutokana na hali hiyo, aliwatahadharisha maofisa ardhi na mipango miji wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kutoa taarifa za uongo katika hatua ya upimaji ardhi, uthamini na utoaji fidia kwa wananchi ambao huuza kwa watu zaidi ya mmoja na kusababisha migogoro usioisha kwa wananchi.
Sitakubali kukaa na watumishi wa vigogo wasioweza kufanya kazi kutatika mkoa huu ,ninafahamu watumishi waliofika Dar es Salaam kwa vimemo ukiuliza ameletwa na kigogo yupo Tamisemi nitawangoa tu,”alisema.

Mkuu huyo bado anaendeleza na ziara yake katika sehemu mbalimbali za wilaya ya Ilala.

Wafuasi wa Trump wakerwa na uamuzi kuhusu Clinton

Wafuasi wahafidhina wa rais mteule wa Marekani Donald Trump wamelalamikia uamuzi wa kiongozi huyo wa kutofuatilia uchunguzi mpya kuhusu kashfa ya barua pepe iliyomkabili mpinzani wake Hillary Clinton.

Maafisa wake walitangaza Jumanne kwamba hatafuatilia ahadi yake ya kuhakikisha Bi Clinton anafungwa jela.

FBI walimuondolea Bi Clinton makosa lakini wafuasi wa Bw Trump walikuwa wakiimba "lock her up" (mfunge jela) kwenye mikutano yake ya kampeni.

Wafuasi wahafidhina sasa wanasema hatua hiyo ya Bw Trump ni "usaliti" na kwamba amevunja ahadi yake.

Tovuti ya Redstate.com imesema hatua ya Bw Trump kutomteua mwendesha mashtaka maalum wa kufuatilia tuhuma hizo dhidi ya Bi Clinton, kama alivyokuwa ameahidi, itafichua "ukweli kwamba yeye ni mtu aliyejidai kuwa wakati wa kampeni".

Tovuti ya mrengo wa kulia ya Breitbart News Network, moja ya tovuti za habari zinazomuunga mkono sana Bw Trump pia ilishutumu hatua hiyo na kusema ni "ahadi iliyovunjwa".



Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Ann Coulter, ambaye ni mhafidhina, aliandika kwenye Twitter: "Whoa! Nilidhani tulimchagua @realDonaldTrump kuwa rais. Tulimfanya FBI, & DOJ? Kazi yake ni kuwateua, si kufanya kazi yao."

Kisha, alifuatiliza kwa ujumbe mwingine: "Hakuna rais anayefaa kuwa akiwazuia wachunguzi kufanya kazi yao. #EqualUnderLaw (Wote sawa mbele ya sheria)"

Shirika la kisheria linaloegemea sasa za mrengo wa kulia la Judicial Watch lilisema huo ni usaliti kwa Wamarekani kuhusu "ahadi yake kwa Wamarekani ya kuondoa maji yote kutoka kwa 'kinamasi' cha ufisadi uliokithiri Washington

Bw Trump baadaye alifafanua na kusema hatua kama hiyo inaweza kuzua migawanyiko zaidi.
FBI walimuondolea Bi Clinton makosa lakini wafuasi wa Bw Trump walikuwa wakiimba "lock her up" (mfunge jela) kwenye mikutano yake ya kampeni.

Wakati wa kampeni, Bw Trump alisema mpinzani wake alikuwa mtu mwovu sana na kuapa kwamba angehakikisha kesi zinafunguliwa dhidi yake.

Alimweleza kama mgombea mfisadi zaidi kuwahi kuwania urais nchini Marekani.
Lakini tangu uchaguzi kumalizika, alionekana kuanza kulegeza msimamo.
Wiki moja iliyopita, alisema familia ya Clinton ni ya "watu wema".

Kisha, Jumanne asubuhi, msemaji wake Kellyanne Conway alisema hakutakuwa na uchunguzi zaidi kuhusu barua pepe za Bi Clinton ili kumpa nafasi ya "kupona".

Saa chache baadaye, Bw Trump mwenyewe aliambia New York Times kwamba uchunguzi mpya haujafutiliwa kabisa lakini hakuna uwezekano mkubwa wa hilo kufanyika kwani litazua migawanyiko zaidi.

"Nataka kusonga mbele. Sitaki kurudi nyuma. Sitaku kuumiza familia ya Clinton, sitaki kamwe."
Kwenye mahojiano na New York Time, Bw Trump pia alijitenga na kundi la watu wanaotetea ubabe wa watu weupe (Wazungu) ambao walipiga saluti za Nazi wakisherehekea ushindi wake mjini Washington Jumamosi

Wasichana waanza kuendesha baiskeli Misri

Wasichana kaskazini mwa Misri wamezindua kampeini ya uendeshaji baiskeli, kupinga maoni potuvu miongoni wanawake wanaoendesha baiskeli.

Si kawaida kumuona mwanamke akiendesha baiskeli nchini Misri, na wale wachache ambao hupeleka husumbuliwa na wapiti njia. Lakini wasichana watano wanajaribu kubadili dhana hiyo.

Wamebuni kundi kwa jina 'hakuna tofauti'' ili kuwaimarisha uendeshaji kama njia mbadala kwa wanawake wanaosafiri, kutokana na ongezeko kubwa la bei ya texi na mabasi madogo tangu serikali walipopunguza ruzuku ya mafuta
.
Hafla ya kwanza, ilikuwa uendeshaji wa baiskeli iliyo jumuisha watu wengi katika mji wa pwani uliowavutia wanawake na wanaume.'' Tunataka kuonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya wanaume na wasichana ,'' Isra Fayed mmoja wa waandalizi alisema hayo kupitia kituo cha televisheni cha serikali cha Al -Qanal.

''Wasichana wana uwezo wa kupeleka baiskeli,na lengo letu la kwanza ni kumahamasisha jamii kuzoea kuwaona wanawake kwenye baiskeli.''

Mradi huo umeungwa mkono na kundi la kutetea haki za wanawake la Kahilah. Muanzilishi wa kundi hilo Enas al-Maasarawy amesema mamia ya vijana wamejiunga na kampeni hiyo ya undeshaji wa baiskeli.

''Kumeshuhudia kiwango kikubwa cha watu.Ni mwanzo wa mabadiliko, Enas al-Maasarawy aliiambia BBC.

Kumekuwa na pongezi nyingi katika ukurasa wa Facebook wa mradi huo, ambapo msichana mmoja kati ya walioshiriki alisema wameungana kwa lengo moja: kuihamasisha jamii kuamini kwamba uendeshaji wa baiskeli ni jambo la kawaida,na hakuna sababu ya kuona haya.

Kumekuwa na maswala mengi kuhusiana na haki za wanawake nchini misri kwa miaka ya hivi karibuni baada ya maswala ya unyanyasaji wa kijinsia na vita dhidi ya wanawake kufuatia mageuzi ya mwaka 2011
. Adhabu kali zilianzishwa mwaka 2014 ikiwemo kifungo jela cha hadi miaka mitano.chanzo bbc swahili

Samatta na Wanyama watemwa orodha ya CAF 2016...

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya wachezaji watano watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016, kwa wachezaji wa jumla na wachezaji wa ligi za barani Afrika.
Wanaoshindania tuzo ya jumla ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka ni:
  • Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borrusia Dortmund
  • Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester
  • Sadio Mane wa Senegal na Liverpool
  • Mohamed Salah wa Egypt na Roma
  • Islam Slimani wa Algeria na Leiceste.Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea soka ya kulipwa Ubelgiji Mbwana Ally Samatta ni miongoni mwa wachezaji 30 waliokuwa wameteuliwa kushindania Tuzo ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ya Mchezaji Bora wa Afrika katika awamu ya kwanza kabla ya wachezaji hao kupunguzwa hadi watano.

    Mkenya Victor Wanyama ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Tottenham alikuwa pia ameteuliwa, pamoja na Yannick Bolasie wa DR Congo anayechezea Everton
    .
    Wachezaji watakaoshindania orodha ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka
    anayecheza ligi za Afrika ni:
  • Khama Billiat wa Mamelodi Sundowns na Zimbabwe
  • Keegan Dolly wa Mamelodi Sundowns na South Africa
  • Rainford Kalaba wa TP Mazembe na Zambia
  • Hlompho Kekana wa Mamelodi Sundowns na South Africa
  • Denis Onyango wa Mamelodi Sundowns na Uganda
  • Wachezaji hao waliamuliwa kwa kura zilizopigwa na Kamati ya Wanahabari ya CAF, Kamati ya Kiufundi na Ustawishaji ya CAF na nusu ya wanachama wa jopo la wataalamu 20.
  • Samatta afurahia kushindania tuzo ya Afrika
  • Samatta na Wanyama kushindania tuzo ya CAF
  • Samatta asaidia klabu yake kufunga
Kwa awamu ya mwisho, kura za makocha wa timu za taifa/wakurugezi wa kiufundi wa mashirikisho 54 ya kitaifa yaliyo wanachama wa CAF pamoja na wanachama washirika - Visiwa vya Reunion na Zanzibar -, kwa pamoja na nsu hiyo nyngine ya wanachama wa jopo la wataalamu 20 zitahesabiwa kuamua washindi.Mshindi atatangazwa Abuja, Nigeria Alhamisi, 5 Januari 2017


Kuna hali mzozo ndani ya magereza ya Uholanzi kutokana na uhaba wa wafungwa..

Huku maeneo mengi ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa kupita kiasi, Uholanzi ina tatizo tofauti . Uchache wa wafungwa . Katika kipindi cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake na mengine zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili liliwezekana - na kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya mahabusu na katika jengo zima . Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao cha jioni . Mwnamume mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliofungwa juu.
"Hawawezi kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel, naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "Lakini wanaweza kuazima visu vidogo vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini"
Baadhi ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya kawaida mara baada ya kufunguliwa.Katikka magereza ya Uholanzi tuanaangalia kila mmoja ," anasema Van der Spoel.
" Kama mtu fulani ana matatizo ya mihadarati tunatibu hali yake, kama ni wenye hasira tunawapatia ushauri wa kudhibiti hasira zao , kama wana matatizo ya pesa tunawapatia ushauri nasaha. Kwa hiyo tunajaribu kuondoa kile kinachosababisha mtu afanye uhalifu . Mfungwa mwenyewe lazima awe na utashi wa kubadilika lakini njia yetu imewafaa sana. Kwa zaidi ya miaka 10 , kazi yetu imeboreka zaidi na zaidi.''
Wafungwa wanaofuata maelekezo hatimaye hupewa kifungo cha miaka miwili na msururu wa mafunzo katika mpango wa kuwarejesha katika hali ya kawaidi . Chini ya 10% hurejea gerezani baada ya kuachiliwa huru.
Hewa safi ni muhimu kwa hiyo wafungwa huruhusiwa kutembea wakisindikizwa hadi maktaba , kwenye kliniki ama mgahawa na hilo huwasaidia kuendelea na maisha ya kawaida punde wanapomaliza kifungo cha gerezani.chanzo na bbc swahili

Kundi la upinzani lamtaka Kabila kujiuzulu...

Kundi la wanaharakati nchini DR Congo limeanzisha kampeni mpya ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kung'atuka mamlakani kulingana na ripoti za BBC Afrique.

Muhula wa pili wa kabila na wa mwisho kwa ujumla unakamilika tarehe 19 Disemba na wapiga kura wanatarajiwa kushiriki katika shughuli hiyo mnamo tarehe 27 Novemba ili kumchagua mrithi wake,lakini makubaliano ya kisiasa yalioafikiwa mwezi uliopita na kundi moja la upinzani yaliahirisha uchaguzi huo hadi mwezi Aprili 2018.

Lakini ukipinga makubaliano hayo muungano wa vuguvugu la kidemokrasia ulizindua kampeni ya ''Bye-Bye Kabila'' ili kumshinikiza kung'atuka muhula wake unapokamilika mwezi Disemba.

Mavuguvugu yalio nyuma ya kampeni hiyo -Filimbi,Lucha na Jeunesse du Rassemblement yamesema kuwa yataandaa maandamano dhidi ya serikali.

Hatua hiyo huenda ikasababisha makabiliano makali na vikosi vya usalama.

Mnamo mwezi Septemba,msako dhidi ya wale wanaoipnga serikali ulisababisha vifo vya watu 50
.
Marie-Joel Essengo,kiongozi wa vuguvugu la Lucha aliambia BBC Afrique:Tutafanya maandamano ili kuwahamasisha miongoni mwa vijana ,katika uma wote hadi tutakapopata mabadiliko tunayohitaji.

Hatuwezi kusubiri na kufikiria kwamba bw. Kabila atepewa dakika moja ya ziada kuwa rais baada ya tarehe 19 Disemba.chanzo na bbc swahili
.

Tuesday, November 22, 2016

VideoMPYA: Davido katuletea hii ‘coolest kid in Africa’ ft. Nasty C


Davido ni miongoni mwa waimbaji wa kizazi cha sasa Afrika ambao hupata attention kubwa kila watu wanaposikia kuna wimbo mpya, hapa katuletea video yake mpya aliyomshirikisha Nasty CCoolest kid in Africa‘ ndio hii hapa chini na ukishaitazama sio mbaya ukiacha comment yako ulivyoipokea

Mawakili Kesi ya Godbless Lema Wagonga Mwamba Mahakamani ......Arudishwa Tena mahabusu ya Gereza la Kisongo

Mbunge  wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kusota katika mahabusu ya Gereza la Kisongo mjini Arusha akiingiza siku ya 22 leo baada ya jana kukwama katika azma yake ya kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliomnyima dhamana.
 

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi ndiye aliyetupilia mbali ombi la Lema, hivyo kumfanya arejee mahabusu huku mawakili wake wakihaha kuhakikisha wanakata rufaa ili kuomba dhamana hiyo katika ngazi nyingine ya kisheria.
 

Aidha, Jaji Moshi ameridhia ombi la Lema kupitia kwa mawakili wake Sheck Mfinanga na Peter Kibatala la kukata rufaa mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.
 

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Jaji Moshi alisema kimsingi hoja ya mawakili wa Lema ya kutaka mahakama hiyo kuitisha faili na kulipitia haina msingi wowote kisheria hivyo anaitupilia mbali hoja hiyo na kutoa rai kwa mawakili hao kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ili dhamana ya Lema isikilizwe
.

“Mahakama hii haiwezi kupitia faili la kesi hii ya Lema ya kupata dhamana hivyo siwezi kupitia faili hili, bali nashauri mkate rufaa ili iweze kusikilizwa,” alisema Jaji Moshi.

Awali Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu la kuitaka wasisikilize maombi ya Lema ya kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 kwa madai yapo makosa ya kisheria yaliyofanywa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.
 

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Moshi katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Kadushi akisaidiana na Materu Marandu alisema anawasilisha hoja mbili za pingamizi za mahakama hiyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo.
Alisema kimsingi maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 yanakinzana na kifungu cha 43 (2) cha sheria ya Mahakama ya Mahakimu. Katika kesi hiyo, Lema anashitakiwa kwa kutoa maneno ya kumtusi Rais katika maeneo tofauti.
 
 

Kadushi alisema uamuzi unaopinga kufanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kukubali kutompa dhamana Lema ni uamuzi mdogo na haukuwa na sababu za kukataa dhamana.

“Mahakama yako inafungwa mikono na kifungu hiki kufanya mapitio au uamuzi mdogo, hivyo tunaomba mahakama itupilie mbali maombi hayo,”alisema Kadushi ambaye wakati akiwasilisha hoja zake alikuwa akinukuu mashauri mbalimbali ya kesi zinazofanana na hiyo.
 

Aidha, Kadushi alisisitiza kuwa wao wanatambua haki ya kukata rufaa ipo wazi kwa mleta maombi ila itakuwa jambo geni kama mahakama itawapa nafasi kusikiliza maombi yao.
 Alisema hoja ya pili ya pingamizi lake, linatokana na mleta maombi kutokidhi matakwa ya kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
 
Aidha, Kadushi alisisitiza kuwa wao wanatambua haki ya kukata rufaa ipo wazi kwa mleta maombi ila itakuwa jambo geni kama mahakama itawapa nafasi kusikiliza maombi yao.
 Alisema hoja ya pili ya pingamizi lake, linatokana na mleta maombi kutokidhi matakwa ya kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Katika sheria ya makosa ya jinai, kifungu cha 359(1) ya mwaka 2002 kuwa mtu asiporidhika na maamuzi ya mahakama ya chini kama ilivyo katika kesi hiyo, kamwe hawezi kuwa na mbadala wa mapitio ya rufaa.

Akijibu hoja hizo Wakili anayemtetea Lema, Peter Kibatala akiwa na jopo la mawakili wenzake, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, John Mallya, Faraji Mangula na Charles Adiel, alipinga kuwekewa pingamizi hilo na kuomba mahakama isikilize maombi yao.

Alisema wao wamefungua maombi hayo kuiomba Mahakama Kuu kuitisha jalada la kesi ya mahakama ya chini ili kuona uhalali wa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kutoa dhamana, kwani kilichokuwa kinasubiriwa ni masharti ya dhamana.

“Huyu mshitakiwa alipewa dhamana , ila kabla ya mahakama haijatoa masharti ya dhamana, upande wa serikali ukasimama kabla mahakama haijaweka masharti ya dhamana ambayo lazima ifanye hivyo, wakasema wameonesha nia ya kukata rufaa na mahakama ikakubaliana nao bila kutekeleza amri yao,” alisema Kibatala.
Aliomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi la serikali na kuiomba kuendelea na kazi iliyokusudia kuifanya ya kupitia maombi yao ili kutoa dhamana kwa mshtakiwa au iamuru mahakama ya chini kuendelea na uamuzi wake.

Wakili wa mbunge huyo baada ya maombi yao kugonga mwamba, walikuwa kwenye hekaheka ya kukamilisha kuandika rufaa ili kumnasua Lema atoke mahabusu.

Baada ya kutoka nje ya Mahakama Kuu, Wakili Mfinanga alisema wanamalizia kukamilisha taratibu za wao kukata rufaa Mahakama Kuu na wataomba rufaa hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura ili kumnasua Lema mahabusu.
 

Jeshi La Polisi Laanza Uchunguzi Dhidi ya Mteja wa NMB Alivyofuatiliwa baada Ya Kutoka Benk na Kuporwa Milioni 15

Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi namna mtu mmoja alivyofuatiliwa na watu wasiojulikana alipotoka benki kuchukua fedha hadi wakampora mfuko uliokuwa na kiasi cha Sh15 milioni muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwake
 
Naibu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku alisema wana taarifa za tukio la wizi huo uliofanyika Ijumaa iliyopita baada ya mteja huyo  kutoka Benki ya NMB Tabata na wanalifanyia kazi kubaini wahalifu hao
Tukio hilo ni moja ya matukio ambayo katika siku za karibuni watu mbalimbali wamekuwa wakiporwa fedha na watu wenye silaha, ikiwa ni muda mfupi baada ya kutoka benki, hali ambayo inajenga wasiwasi juu ya sehemu ambmuda mfupi baada ya kutoka benki, hali ambayo inajenga wasiwasi juu ya sehemu ambazo majambazi hao hupata taarifa za watu wanaokwenda benki kuchukua fedha.
 
Hofu miongoni mwa wateja imezidi kutokana na tukio lililotokea Ijumaa ya wiki iliyopita ambapo majambazi wakiwa na pikipiki mbili walimfuatilia mteja aliyetoka kuchukua fedha benki kiasi cha Sh15 milioni na kumpora mbele ya nyumba yake. 
Akisimulia tukio hilo mwathiri- ka wa wizi huo, alisema alichukua fedha kwenye tawi la NMB Tabata kisha akapanda daladala akaenda kushuka kituo cha Tabata Bima. 
Alisema alipokuwa anaelekea nyumbani kwake hakuwa na shaka, lakini alipokaribia alihisi kuna mtu anamfuata ingawa hakumuona, hivyo aliingia kwenye baa iliyokuwa njiani na kutokea upande wa pili kwa kutumia uchochoro uliokuwapo. 
Alisema baada ya kutokea upande wa pili aliangaza kushoto na kulia hakuona mtu kisha aliamua kuongoza hadi nyumbani kwake.azo majambazi hao hupata taarifa za watu wanaokwenda benki kuchukua fedha.
Alisema baada ya kutokea upande wa pili aliangaza kushoto na kulia hakuona mtu kisha aliamua kuongoza hadi nyumbani kwake. 
“Nilipofika hapo nje kwenye mwembe (umbali wa mita tatu kuingia ndani ya nyumba yake), nikakuta watu wanne wakiwa na pikipiki mbili wamesimama mbele yangu,” alisimulia akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kuruhusiwa Hospitali ya Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu. 
“Wakanitaka niwape fedha ambazo zilikuwa kwenye mfuko nimezishika mkononi. Kabla sijakaa vizuri wakapiga risasi hewani, kutahamaki wakanipiga juu ya goti la mguu wa kulia ikaniparaza, lakini nilikuwa bado nimeng’ang’ania ule mfuko wenye fedha,” alisema.
 
Aliendelea kueleza kuwa baada ya kuona hana mpango wa kutoa fedha, wakampiga risasi mguu huo huo chini ya goti ikapasua mfupa mkubwa na kutokea upande wa pili na kumnyang’anya mfuko wa fedha.Hakuna mtu aliyekuwa anafahamu suala hilo zaidi ya mimi mwenyewe,” alisema huku akiugulia maumivu

 

UN yaendelea kutoa misaada kwa wakimbizi wa Syria...

Umoja wa mataifa umeendelea kutoa msaada kwa zaidi ya wakimbizi elfu hamsini na nane wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto Baada ya vikosi vya Jordan kujitoa kuisaidia Syria.

Wamekuwa wakiishi kwa awamu mbili kambini katika maeneo ya pembezoni.

Jordan ilifunga mipaka yake kufuatia shambulizi la mabomu lililouwa wanajeshi saba mwezi June mwaka huu, ambapo wapiganaji wa kiislam walihusishwa na tukio hili, chakula kwa wakimbizi kimepelekwa mara moja.

Umoja wa mataifa unatarajia kujenga hospitali ya wakimbizi katika kambi hizo.chanzo na bbc swahili.

Cameroon: Vikosi vya usalama vyawatawanya waandamanaji wanaopinga kifaransa...

Nchini Cameroon vikosi vya usalama vimewatawanyisha kwa mabomu ya machozi na risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga serikali Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo
.
Inasemekana kuwa baadhi ya watu wamefariki na wengine kujeruhiwa katika mji wa Bamenda.
Maandamano yalianza siku ya Jumatatu wakiwaunga mkono walimu walikokuwa wakipinga kuanzishwa kwa Lugha ya kifaransa mashuleni katika maeneo yanayozungumza Anglofone huko nchini Cameroon.

Wanasheria wamekuwa wakiandamana kwa kipindi cha wiki mbili kufuatia kuamrishwa na Serikali kutumia lugha ya kifaransa katika masuala ya kisheria.

Wacameroon wengi huzungumza lugha ya kifaransa huku watu wa maeneo yanayozungumza kingereza wamesema wanadharaulika.chanzo bbc swahili.chanzo na bbc swahili
.

Tetemeko lasababisha kimbunga Fukushima, Japan

Tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.4 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Fukushima na Miyagi nchini Japan na kusababisha kimbunga chenye mawimbi ya urefu wa zaidi ya mita moja.

Tetemeko hilo limetokea mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi saa za Japan (21:00 GMT Jumatatu), idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Japan (JMA) imesema.

Wakazi walishauriwa kukimbilia maeneo yaliyo juu upesi, huku mawimbi yakihofiwa kufikia urefu wa mita 3.

Kulikuwa na taarifa za watu kadha kupata majeraha madogo pamoja na uharibifu kutokea.
Tetemeko jingine lilitokea eneo hilo mwaka 2011 na kusababisha kimbunga ambapo watu zaidi ya 18,000 walifariki.

Tetemeko hilo, moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, liliharibu kinu cha nyuklia cha Fukushima. Hadi sasa, shughuli kubwa ya kuondoa taka za nyuklia imekuwa ikiendeleaTetemeko jingine lilitokea eneo hilo mwaka 2011 na kusababisha kimbunga ambapo watu zaidi ya 18,000 walifariki.

Tetemeko hilo, moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, liliharibu kinu cha nyuklia cha Fukushima. Hadi sasa, shughuli kubwa ya kuondoa taka za nyuklia imekuwa ikiendelea.
Maafisa wa serikali wanasema hakujakuwa na dalili zozote za uharibifu kwenye kinu hicho wakati huu.

Maafisa wa Jiolojia wa Marekani awali walikuwa wamekadiria nguvu ya tetemeko hilo kuwa 7.3 lakini baadaye wakapunguza hadi 6.9, kipimo ambacho ni cha chini kuliko kile kilichotolewa na wenzao wa Japan.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Japan inasema tetemeko la sasa linauhusiano na tetemeko la mwaka 2011.

Msemaji mmoja aliyenukuliwa na Japan Times amesema eneo hilo limekuwa likipokea tetemeko la 7.0 angalau mara moja kila mwaka.

Kina cha tetemeko la Jumanne kinakadiriwa kuwa kilomita 30 chini ya ardhi (maili 18.6), JMA imesema.

Mitetemeko mikubwa imesikika maeneo ya mbali yakiwemo mji mkuu New York ulio maili 100 kusini mwa Fukushima.chanzo na bbc swahili

Mwenyekiti aomba kupigwa risasi mbele ya Makonda baada ya kubanwa na Wananchi


Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo
.
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa nafasi kwa wakazi wa Mbande hususan wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.

Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.

Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.

TUCTA yashauri kufanyika uhakiki wa vyeti katika sekta binafsi...


nicholas-mgaya
Katibu Mkuu wa shirikisho (TUCTA), Nicholaus Mgaya.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeunga mkono utaratibu wa serikali wa kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma na kutaka utaratibu huo ufanyike pia kwenye sekta binafsi.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo Jumatatu hii , Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Nicholaus Mgaya alisema uhakiki huo utasaidia kuondoa watumishi wengi wasiowajibika kwa kukosa sifa na kuhakikisha wale wenye sifa ndio wanapata ajira.

“Tunaomba huu uwe utaratibu wa nchi nzima, maeneo yote yaguswe na uhakiki huu kwa sababu ukweli uko wazi kwa sasa kuna watanzania wengi tena wasomi wa hali ya juu hawana ajira lakini nafasi zao zimezibwa na watu wasio na sifa,” alisisitiza Mgaya.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao na Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Yunus Ndaro alisema vyama vya wafanyakazi vinaunga mkono hatua hiyo ya serikali kwani itasaidia kurejesha heshima ya ajira nchini.

Alisema sekta binafsi pia ni sehemu ya Tanzania na inajiendesha pia kwa kufuata Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Mwaka 2004, hivyo nayo inapaswa kuhakikiwa ili kuhakikisha inafuata misingi, kanuni na sheria za nchi.

“Mfano zipo kampuni nyingi za simu baadhi yake zikiwa binafsi zinaingiza wafanyakazi wageni kutoka nje ya nchi, wengi wakiwa hawana sifa, kupitia uhakiki huu haya yote yatavumbuliwa,” alisisitiza Ndaro.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Askofu Dk Owdenburg Mdegella pamoja na kuipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu huo, naye aliomba kufanyike hadi sekta binafsi ili kupunguza ongezeko la vyeti bandia.

TFF imemfungia kocha wa Yanga Hans van Pluijm mechi 3 na kumpiga faini


Shirikisho la soka Tanzania TFF leo November 22 2016 kupitia kwa kamati ya saa 72 imetangaza kumuadhibu kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm kwa tuhuma za kuwatolea lugha chafu waamuzi wa mechi
.
Kamati ya saa 72 imemfungia kocha Hans van Pluijm mechi tatu kukaa katika benchi na kumpiga faini ya Tsh 500,000 kwa kosa hilo, Hans anatajwa kuwatolewa lugha chafu waamuzi wakati wa mchezo na baada ya mchezo kuwafuata katika vyumba vya kubadilishia nguo
.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Hans van Pluijm alioneshwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka kama mchezaji na kama kocha November 10 2016 katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa tuhuma za kupishana kauli na refa.chanzo na millard ayo.

Rio 2016: Afisa ashtakiwa kwa kashfa ya fedha Kenya

Afisa wa tano wa michezo ya Olimpiki nchini Kenya amekamatwa ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi unaozunguka fedha na vifaa vilivyopotea katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio.

Maafisa wa polisi walivamia nyumbani kwa Ben Ekumbo, ambaye ni makamu wa rais wa kamati ya Olimpiki na msimamizi wa shirikisho la waogeleaji.

Aliripotiwa kujificha chini ya kitanda.

Maafisa walipata maboksi ya viatu vya Nike pamoja na jezi ambazo zilikuwa hazijatumiwa ambazo zilipangwa kupewa wanariadha walioshiriki katika michezo hiyo.

Kukamatwa kwake kunajiri baada ya kudaiwa katika ripoti nyengine ya uchunguzi kwamba maafisa wakuu wa michezo waliiba zaidi ya pauni milioni 6.4 ,kama matumizi na vifaa vya wanariadha
.
Maafisa wengine wanne walikamatwa mnamo mwezi Septemba

.
Kiongozi wa ujumbe wa timu ya Kenya katika michezo hiyo Stephen Arap Soi alishtakiwa kwa kuiba dola milioni 250,000 ambazo zingetumika kugharamikia nauli,malazi pamoja na matumizi mengine ya wanariadha mjini Rio.


Makamu mwengine wa shirikisho hilo Pius Ochieng na katibu mkuu Francis Kinyili Paul pia walishtakiwa kwa kuiba jezi za Nike.CHANZO NA BBC SWAHILI

Mtu mwenye HIV aliyefanya mapenzi na wanawake 104 Malawi afungwa miaka 2 jela..

Mahakama moja nchini Malawi imempatia hukumu ya miaka miwili jela mtu mwenye virusi vya HIV ambaye alikiri kufanya tendo la ngono na zaidi ya wanawake 100 na wasichana bila kutangaza hali yake.

Katika uamuzi mkubwa uliotarajiwa na wengi,Eric Aniva alipatikana na hatia ya ''kutekeleza mila zenye madhara'' chini ya sheria za kijinsia za taifa hilo baada ya uchunguzi wa BBC kubaini vile alivyolipwa ili kuwafanyia sherehe za kutakasa wasichana wadogo pamoja na wanawake wajane
.
Eric Aniva ni mwanamume wa kwanza kufungwa jela kuwa 'fisi' neno linalotumika kwa mwanamume anayelipwa ili kushiriki ngono na wanawake pamoja na wasichana ikiwa ni miongoni mwa tamaduni za kutakasa.

Katika mahojiano na BBC ,alikiri kufanya mapenzi na wanawake 104 na wasichana bila kuwalezea kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya HIV
.
Ijapokuwa hakuna msichana aliyejitokeza, kulalamika, alipatikana na hatia ya kutekeleza mila zenye madhara baada ya wanawake wawili kutoa ushahidi wao.

Wote wawili ni wajane ambao wanasema walilazimishwa kufanya mapenzi na mtu huyo ili kutakasa roho za waume zao baada ya vifo vyao.

Kesi hiyo imezua maoni tofauti nchini Malawi huku baadhi yao wakidai kwamba sheria kali za kijinsia zinaingilia utamaduni na kwamba bw Aniva anasulubiwa .

Wakati huohuo mashirika ya haki za kibinaadamu yanaamini kwamba kesi hiyo ni ushindi katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kingono...CHANZO NA BBC SWHILI

Monday, November 21, 2016

Kina dada wa Kenya walazwa 3-1 na Ghana nchini Cameroon..

Harambee StarletsUtata ulikumba mechi ya ufunguzi ya timu ya taifa ya Kenya, Harambee Starlets iliposhindwa mabao 3-1 na Ghana katika mechi ya mchuano wa kuwania kombe la taifa bingwa Afrika kwa upande wa wanawake (Awcon) kufuatia maamuzi tata mjini Limbe usiku wa Jumapili

Esse Mbeyu Akida alikuwa ameiweka Kenya kifua mbele katika kipindi cha kwanza kabla ya utepetevu wa safu ya ulinzi ya Kenya kusababisha Samira Souleyman kusawazishia Ghana mapema baada ya mapumziko.

Hata hivyo refarii Jeanne Ekoumou raia wa Cameroon aliibua hisia kali miongoni mwa timu ya taifa ya Kenya ya wanawake aliponyoosha mkono wake akiashiria mkwaju wa penalti ilhali tukio la utovu wa nidhamu lilikuwa limetokea nje ya eneo la lango
.
Hata hivyo mashabiki waliokuwa uwanjani walighadhabishwa mno na uamuzi huo wa refa Ekoumou baada ya picha za runinga zilizoonyeshwa uwanjani kuonesha wazi kuwa mchezaji wa Kenya aliyeunawa mpira alikuwa nje kabisa ya eneo la lango.

Lakini kama kilio cha kuku ambacho hakimpati mwewe, Ghana hawakuchelea, walifuma mkwaju kimiani na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele wakiongoza mabao 2-1 kunako dakika ya 71 ya kipindi cha pili.

Mfungaji wa tobwe hilo akiwa ni nahodha Elizabeth Addo.
Dakika moja baadaye refarii huyo alichomeka msumari wa moto kwenye kidonda cha Kenya alipopuuzilia mbali ombi la Kenya la penalti mshambulizi Esse Mbeyu Akida alipoangushwa mbele ya lango na walinzi wa Ghana.

Bi Ekoumou akaonesha wazi ishara ya kuwa ni penalty kwa upande wa Kenya.Lakini baada ya dakika chache za majadiliano na msaidizi wake alibadilisha kauli hiyo na kuwapa the Black Queens wa Ghana mkwaju wa adhabu.
 Wakenya waliteta na kubisha lakini wapii Ekoumou alisimama kidete na kupuliza kipenga mpira uendelee.
 Kwanzia hapo ilikuwa bayana kuwa Wakenya walikuwa washapoteza ari ya kucheza na haikuwa ajabu kombora la Portia Boakye lilipotikisa wavu wa Kenya kipa wao Samantha Akinyi akiwa ameduwaa.

Bao hilo la dakika ya 91 ya mechi hiyo ilikuwa msumari wa mwisho katika jeneza la wakenya waliosalia wananongoneza jinsi maamuzi yalivyoponza ndoto yao ya kusunga mbele katika kidumbwedumbwe hicho chao cha kwanza kuwahi kushiriki.


Hayo yalijiri huku mabingwa watetezi Nigeria wakitangaza wazi ari yao kwa kuwanyeshea Mali mabao 6-0 katika mechi ya ufunguzi ya kundi Ba. Mshambulizi wa , Arsenal Asisat Oshoala alifungua kivuno hicho cha mabao kwa kufunga mabao 4 na kuwaongoza Super Falcons kuthibitisha udedea wao.

Kufuatia ushindi huo Super Falcons wanahitaji kuilaza Black Queens ya Ghana katika mechi ijao ilikujihakikishia nafasi katika raundi ya pili ya nusu fainali ya mchuano huo.

Kenya itarejea uwanjani Jumatano tarehe 23 huko huko Limbe Cameroon kumaliza udhia dhidi ya Mali.Kenya itarejea uwanjani Jumatano tarehe 23 huko huko Limbe Cameroon kumaliza udhia dhidi ya Mali.chanzo bbc swahili
.

27 wauawa kwa bomu Kabul wakati wa ibada....

Mlipuaji mabomu wa kujitolea muhanga amejilipua na kuwauwa watu 27 katika msikiti wa waislam wa madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Afghanstan Kabul, wamesema polisi.

Takriban watu 35 zaidi wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokeakatika msikiti wa Baqir ul Olum magharibi mwa mji huo.

Shambulio hilo limekuja wakati waumini walipokuwa wamekusanyika kwa sherehe za kidini.
Kundi la Islamic State (IS) limesema kuwa lilihusika na mlipuko huo.

Ni shambulio la hivi karibuni katika ya msururu wa mashambulio kadhaa ya hivi karibuni yanayolenga jamii ya waislam wa madhehebu ya Shia yanayodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislam wa madhehebu ya Sunni
.
Kundi la Islamic State (IS) limesema kuwa lilihusika na mlipuko huo.

Ni shambulio la hivi karibuni katika ya msururu wa mashambulio kadhaa ya hivi karibuni yanayolenga jamii ya waislam wa madhehebu ya Shia yanayodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislam wa madhehebu ya Sunni.

 
Ulipuaji mabomu huo ulitokea wakati wa ibada ya kumbu kumbu ya kifo cha Imam Hussein, mjukuu wa Mtume Muhammad ambaye pia ni mfiadini wa kishia
.
Maafisa wanasema kuwa mshambuliaji alikuwa anatembea kwa miguu na kujilipua miongoni mwa umati wa watu wwaliokuwa nje ya jengo . Walioshuhudia wanasema alijilipua wakati ibada ilipokuwa kalibu kukamilika