.Moja kati ya michezo iliyochezwa siku ya May 15 ni mchezo kati ya timu ya taifa ya Mali ambao ndio Mabingwa watetezi dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Serengeti Boys, mchezo huo wengi walikuwa wakitarajia kuona Mali akifanikiwa kuondoka na point tatu ukilinganisha lakini walijikuta game ikimalizika kwa sare tasa 0-0.
Rekodi ni nyingi zilizokuwa zinambeba Mali ambaye ndio Bingwa mtetezi wa michuano ambapo alitwaa taji hilo 2015 akiwa kacheza jumla ya michezo mitano na kutofungwa katika michezo yote zaidi ya kuishia sare mchezo mmoja dhidi ya Afrika Kusini February 19 2015 ilikuwa sare ya 2-2 na kuambulia kufunga jumla ya magoli 10 na kuruhusu kufungwa magoli manne
.Baada ya game hiyo mchezo wa pili wa kundi hilo kati ya Angola dhidi ya Niger ulichezwa na kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, matokeo hayo yamelifanya Kundi B kuwa bado gumu kutokana na kila mmoja kuwa na point moja, Tanzania itashuka dimbani tarehe 18 kucheza dhidi ya Angola wakati Mali watacheza dhidi ya Niger siku hiyo
No comments:
Post a Comment