Tuesday, May 16, 2017

TANZANIA YANGARA MICHUANO KIMATAIFA

Baada ya May 14 2017 michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kuanza nchini Gabon katika uwanja wa Port Gentil, May 15 ilikuwa ni zamu ya michezo ya Kundi B kuchezwa katika uwanja wa Stade de Amitie jijini Libreville kwa michezo Kundi B kuchezwa
.Moja kati ya michezo iliyochezwa siku ya May 15 ni mchezo kati ya timu ya taifa ya Mali ambao ndio Mabingwa watetezi dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Serengeti Boys, mchezo huo wengi walikuwa wakitarajia kuona Mali akifanikiwa kuondoka na point tatu ukilinganisha lakini walijikuta game ikimalizika kwa sare tasa 0-0.

Rekodi ni nyingi zilizokuwa zinambeba Mali ambaye ndio Bingwa mtetezi wa michuano ambapo alitwaa taji hilo 2015 akiwa kacheza jumla ya michezo mitano na kutofungwa katika michezo yote zaidi ya kuishia sare mchezo mmoja dhidi ya Afrika Kusini February 19 2015 ilikuwa sare ya 2-2 na kuambulia kufunga jumla ya magoli 10 na kuruhusu kufungwa magoli manne
.Baada ya game hiyo mchezo  wa pili wa kundi hilo kati ya Angola dhidi ya Niger ulichezwa na kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, matokeo hayo yamelifanya Kundi B kuwa bado gumu kutokana na kila mmoja kuwa na point moja, Tanzania itashuka dimbani tarehe 18 kucheza dhidi ya Angola wakati Mali watacheza dhidi ya Niger siku hiyo

Upinzani Kenya watishia kususia uchaguzi mkuu

Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa mrengo wa upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.
IEBC imeijibu mrengo wa upinzani wa Nasa kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioruhusu matokeo ya kura za Urais kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.
Hii ni baada ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za kubadili mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika kituo cha kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.Tume hiyo kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.
Viongozi wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga, walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangzwa kitaifa.
''Kuitishia IEBC kuhusu uamuzi wake wa kukata rufaa, ni kutishia uhuru wake, na wasioridishwa na hatua hiyo, wajiunge kwenye kesi wasake suluhisho za kisheria,'' alisema Chebukati.
Taifa la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa Upinzani wa Nasa.Takriban wagombea kumi na wanane wa Urais wamejitokeza.chanzo na bbc swahili

Kijana wa miaka 17 auawa katika maandamano Venezuela

Kijana mdogo ameuawa nchini Venezuela katika siku nyingine ya maandamano dhidi ya Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro, maandamano ambayo kwa sasa yanazorotesha uchumi wa taifa hilo.
Kijana mwenye umri wa miaka 17, Luis Alviarez alipigwa risasi kifuani katika maandamano ya upinzani kwenye mji wa Guasimo, Mashariki mwa nchi hiyo.
Wito umetolewa wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mazingira ya mauaji hayo.Kiongozi wa wanafunzi mwenye umri wa miaka 22 Wilmer Arevalo naye yu mahututi baada ya kupigwa risasi kichwani kwenye maandamano mengine.
Pia kwenye jimbo la Tachira, wanaharakati wapinzani wa shirika la Foro penal wamesema zaidi ya watu 40 walikamatwa siku ya jumatatu .
Takriban watu 40 wameuawa tangu maandamano kuanza nchini humo majuma saba yaliyopita.chanzo na bbc swahili

Mwanahabari mfichuzi wa mihadarati auwawa Mexico

Mwaandishi habari aliyeshinda matuzo mengi kuhusiana na taarifa zake nyingi ya ufichuzi wa shughuli za makundi, yanayojihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico, ameuwawa.
Javier Valdez, aliuwawa na watu wenye silaha ambao walimiminia gari lake risasi akiwa katika mji wa Culiacán- jimbo la Sinaloa, kaskazini mwa nchi hiyo.
Javier Valdez aliuwawa alipokuwa akiliendesha gari lake kwenda ofisini kuliko na mtandao wake wa habari alilolianzisha huko Rio Doce.Pia aliifanyia kazi shirika la habari la AFP, na gazeti moja maarufu nchini Mexico- La Jornada.
Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, ameamuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na kile alichosema uhalifu wa kutisha.
AFP nayo inasema kuwa Bwana Valdez alikuwa ameonyesha utendaki wa hali ya juu ya upekuzi dhidi ya walanguzi wa mihadarati, licha ya kufahamu kuwa alikuwa anahatarisha maisha yake.
Waandishi wanne wameuwawa nchini Mexico, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita

JONHN TERRY KUIGA SOKA SASA

Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amesema kuwa huenda akastaafu baada ya kuwasaidia mabingwa hao wapya wa EPL kuilaza Watford kwa magoli 4-3 dimbani Stamford Bridge.
Terry mwenye miaka 36 ambaye amefunga goli la kwanza katika mchezo huo, ataondoka mwishoni mwa msimu huuChelsea watakuwa wenyeji wa Sunderland siku ya Jumapili hii ikiwa ni mchezo wa mwisho kabisa kwa msimu huu.
Terry ameichezea Chelsea michezo 716 hii ikiwa ni tokea mwaka 1998.
Ameisaidia Chelsea kushinda vikombe vitano vya FA, Vitatu vya Ligi ya EPL, kombe la mabingwa Ulaya mara moja na Europa ligi mara 1