Tuesday, August 23, 2016

WANAFUNZI WATAKIWA KUWEKA JITIHADA KATIKA MASOMO YAO

 Wanafunzi wachuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha  wametakiwa kuweka juhudu katika masomo ya vitendo na nadharia ili kuweza kuimarika katika tasinia ya habari.

Hayo yamesemwa na mkufunzi wa chuo hicho Bw . Onesimo Mbise wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo.

Mbise amesem kuwa wanafunzi wanapaswa kusoma kwa bidii na kufanya mrejesho kile wanachofundisha darasani ili kuweza kuwana ufaulu mzuri katika mitihani yao,

Aidha ameongezea kwa kusema kuwa  kutokana na wanafunzi chuoni hapo kuwa na ujuzi katika masomo kivitendo wakufunzi wameamua kuweka nguvu kazi kwa upande wa masomo ya nadharia ikiwa ni pamoja ufanyaji wa mitihani kila siku.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi akiwemo Frolah Kashenye amesema kuwa zoezi la ufanyaji mitihani ni nzuri kwani litawaongezea ufanisi zaidi pamoja na uelewa wa kutosha katika tasinia hiyo.

Amehitimisha kwa kuwasihi wanafunzi chuoni hapo kuwa nidhanimu pamoja na kuhudhuria masomo kwani kupitia mitihani wanayofanya wataweza kukamilisha ndoto zao,

No comments:

Post a Comment